Sam Allardyce ameteuliwa kuwa kocha mpya wa
timu ya taifa ya Engand, hii ni kwa mujibu wa
taarifa kutoka Chama Cha Soka England (FA).
Allardyce (61) amechukua jukumu la kuinoa timu
hiyo maarufu kama ‘Three Lions’ kufuatia
kujiuzulu kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Roy
Hodgson baada ya kutolewa na Iceland katika
Michuano ya Euro mwaka huu iliyomalizika hivi
karibuni nchini Ufaransa.
Allardyce amepata nafasi baada ya kumshinda
kocha wa Hull City Steve Bruce na kocha wa
Marekani Jurgen Klinsmann
Kocha huyo wa zamani wa Bolton Wanderers,
Blackburn Rovers na West Ham United ameacha
kazi kwenye klabu ya Sunderland kufuatia ya
kuinusuru kutoshuka daraja msimu uliopita baada
ya kudumu kalbuni hapo kwa miezi tisa tu.
Amefurahia sana uteuzi huo na kusema kwamba
“Sasa ni muda wa kutoa kile alichonacho”.
“Nimefurahi sana kuteuliwa kuwa kocha wa
England hasa kutokana na ukweli kwamba bila ya
kuificha hii ni kazi ambayo kwa muda mrefu sana
nimekuwa nikiihitaji. Kwangu mimi, hii ni kazi
bora kabisa kwenye tasnia ya soka nchini
England.” aliiambia tovuti ya FA.
“Nitafanya kila liwezekanalo ili kuisaidia England
kufanya vizuri na kuwapa furaha mashabiki wetu,
na zaidi ya yote ni kuwafanya wajivunie utaifa
wao.”
“Wakati mawazo yangu yote yatakuwa kwenye
timu ya wakubwa na kupata matokeo mazuri,
nataka niongeze ushawishi wangu mpaka kwenye
timu za vijana.”
“Najua tuna vipaji vingi, tuna wachezaji ambao
wana moyo wa dhati wa kulitumikia taifa lao na
sasa ni muda muafaka wa kuwapa mashabiki wetu
furaha.
Mtihani wa kwanza wa Allardyce utakuwa ni
Septemba 4 wakati England watakapovaana na
Slovakia.”
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni