ni kucheza kwa mara ya kwanza michuano ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kufanikiwa
kutinga Uropa
Nyota huyo wa kimataifa wa Tanzania
ameonyesha thamani yake kwa klabu
anayoichezea Ubelgiji Genk, kwani amekuwa
akifunga magoli muhimu kila anapopata fursa.
Kwa mujibu wa Bin Zubeiry Sports -
Online baada ya timu yake kuitoa Buducnost ya
Montenegro kwa penalti 4-2 Uwanja wa Pod
Goricom mjini Podgorica katika mchezo wa
marudiano Raundi ya Pili ya mchujo wa kufuzu
hatua ya makundi ya Europ League, Samatta
alisema kwamba amefurahi kwa matokeo hayo na
sasa anaangalia mbele kuisaidia zaidi Genk ili
ifike mbali kwenye michuano hiyo.
“Kwa kweli nimejisikia vizuri, maana ngoma
ilikuwa ngumu na pia ninajisikia vyema, kwani
ninazidi kupata uzoefu wa mashindano tofauti pia
ni kitu kinachonifanya nionekane sehemu nyingi
tofauti,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani
wa African Lyon na Simba SC za Dar es Salaam.
“Matarajio yetu kama timu ni kuwa na kipindi
chenye mafanikio ndani ya msimu huu, nami
binafsi kama mimi napenda ndani ya msimu huu
niwe na rekodi nzuri za mabao na wastani mzuri
wa mechi na kuisaidia timu yangu kushiriki Ligi
ya Mabingwa Ulaya mwakani,” alisema Samatta.
Chapisha Maoni