Nahodha wa Klabu ya Yanga Nadir Haroub
Cannavaro amesema, mchezo wa marudiano dhidi
ya Medeama ni mgumu lakini ushindi pia kwa
upande wao ni lazima ili kuweza kujiweka katika
hali ya usalama katika hatua ya makundi ya kombe
la shirikisho barani Afrika.
Cannavaro amesema, licha ya kupoteza michezo
miwili na kutoa sare mchezo mmoja lakini
hawawezi kukata tamaa katika safari ya kuwania
kusonga mbele katika michuano hiyo kwani bado
wanaamini nafasi ipo.
Cannavaro amesema, kocha ameangalia
mapungufu yaliyojitokeza katika michezo iliyopita
na ameyafanyia marekebisho ili kuweza kukiweka
kikosi katika uimara zaidi kwa ajili ya mchezo wa
marudiano siku ya jumanne.
Yanga imeondoka Alfajiri ya jana kuelekea nchini
Ghana kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa hatua
ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika dhidi ya
timu ya Medeama utakaopigwa Jumanne ya Julai
26.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni