0
Inasikitisha lakini ndio ukweli kwamba
Silvio Berlusconi ameiuza timu ya AC
Milan. Timu hiyo sasa imenunuliwa na
mmliki wa kampuni ya Baidu kutoka
China yenye kumilikiwa na bilionea
Robin Li.
Hii ni baada ya timu ya Inter Milan ya
mjini Milan nchini Italia kununuliwa na
kampuni kutoka China ya Suning, na
sasa hatimaye mwenyekiti wa timu
nyingine ya mjini Milan, AC Milan, Silvio
Berlusconi naye akaamua kuachia ngazi
na kuiuza timu hiyo kwa kampuni ya
Baidu kutoka China kwa kitita cha dola
milioni 437 sawa na hisa asilimia 70 za
timu hiyo na kuachia hisa asilimia 30 tu
kwa kampuni ya Fininvest inayomilikiwa
na mwenyekiti huyo.
Habari hizi zilifahamishwa na vyombo
vya habari vya nchi za Italia na China.

Chapisha Maoni

 
Top