0

MO anataka kubadili mwenendo wa timu hiyo na
kuiendesha kisasa kama ilivyo klabu ya TP
Mazembe na nyinginezo zinazofanya vizuri Afrika
Klabu ya Simba leo inatarajiwa kuchukua
maamuzi magumu kwa kukubali kumpa timu
Bilionea Mohamed Dewji, ‘MO’, kama mmiliki wa
timu hiyo kutokana na uwekezaji wake wa Bilioni
20 anaotaka kuwekeza.
Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva, leo
anakutana na wanachama wa klabu hiyo kujadili
swala hilo na jibu litakalopatikana kama kukubali
au kukataa litajulikana leo lakini tajiri huyo
amesema yeye anasubiri majibu hayo na hata
kama ikitokea wamekataa hatoweza kufanya
chochote.
MO amesema anataka kubadili mwenendo wa
timu hiyo na kuiendesha kisasa kama ilivyo
klabu ya TP Mazembe na nyinginezo zinazofanya
vizuri Afrika kwa kutumia bajeti kubwa kwa ajili
ya kuijenga timu.
Bilionea huyo amesema Simba haifanyi vizuri
kwasababu imezidiwa kwa kiasi kikubwa na klabu
za Yanga na Azam na hiyo inatokana bajeti
ndogo wanayotumia.
Mkutano wa Simba unafanyika leo kwenye
ukumbi wa Maofisa wa Polisi Masaki Dar es
Salaam na maamuzi ya kukubali ndiyo yataiibadili
klabu hiyo ambayo imekuwa katika wakati
mgumu wa kushindwa kupata mafanikio katika
misimu mitatu iliyopita.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top