Klabu ya soka ya Yanga na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) zimeendelea kuvutana kuhusu
mapato baada ya mchezo wa Jumamosi ambapo
Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Medeama
ya Ghana.
Baada ya mchezo huo Yanga ilidaiwa kugomea
kulipwa pesa taslimu ikitaka ipewe hundi
Yanga ilitaka fedha zote zipelekwe benki kisha
mgawo upitie mfumo wa hundi.
Kwa kuwa hilo halijazoeleka, TFF iliendelea
kusisitiza malipo yafanyike kwa utaratibu wa
kawaida kuwa zitolewe "cash cash".
Suala hilo baadaye liliamuliwa na Serikali na
inaelezwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ndiye aliyemaliza
ubishi huo kwa kuiunga mkono Yanga.
Yanga ilieleza sababu ya kuchagua mfumo huo ni
ili kutumia mashine za EFD wakati wa malipo na
kutoa risiti kwa kila watakaolipwa.
TFF na Yanga zimekuwa zikiwindana tangu Yanga
iufanya mchezo wake dhidi ya TP Mazembe kuwa
bure wakati TFF ilikuwa imeshatangaza viingilio.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni