0

Klabu ya soka ya ligi kuu ya nchini Uingereza,
Arsenal, imeichapa mabo 3-1, klabu ya Chivas, ya
ligi kuu ya soka ya Mexico, kwenye mchezo wa
kirafiki.
Arsenal imemaliza ziara yake ya nchini Marekani,
kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chivas ya
nchini Mexico, mjini, Los Angeles, Marekani, alfajiri
ya leo.
Mlinzi mpya wa klabu hiyo, Rob Holding, aliifungia
Arsenal bao la kwanza kwenye dakika ya 34, kabla
ya Alex Oxlade-Chamberlain na Chuba Akpom
kuongeza mabao ya kipindi cha pili.
Chivas ilipata bao la kufutia machozi kutoka kwa
mchezaji aliyeingia kutoka benchi, Angel Zaldivar,
akifunga kwa penati, mbele ya watazamaji 25,000
kwenye uwanja wa Stub Hub Center, unaomilikiwa
na klabu ya L.A Galaxy.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top