Baraza la Michezo Tanzania (BMT) lipo katika
mchakato wa kutaka kujiridhisha juu ya tukio la
Rais wa TFF Jamal Malinzi kuamua kugombea
nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa
Kagera wakati akiwa bado ni kiongozi wa juu wa
Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF).
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja
amethibitisha taarifa hiyo: “Tunaangalia katiba zao
zinasemaje kwanza, kwasababu sasahivi bado
tunaangalia historia kwakua viongozi waliopita
hawakufanya hivi. Sijaiona katiba ya chama
alichogombea kule (Kagera) nikijiridhisha nitatoa
majibu.”
Kama BMT itajiridhisha kwamba Malinzi
amegombea kwa mujibu wakanuni na taratibu,
basi atakuwa salama, lakini kama atakuwa nje ya
katiba basi BMT itajua nini cha kufanya.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni