Shirikisho la Soka la Nigeria (NFA), limesogeza
mbele kwa siku moja mchezo kati ya timu ya taifa
ya Nigeria ‘The Super Eagles’ na Tanzania ‘Taifa
Stars’ ambako sasa utafanyika Septemba 3, 2016
badala ya Septemba 2, 2016 iliyotangazwa awali.
Aidha, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles
Boniface Mkwasa kesho anatarajiwa kutangaza
kikosi ambacho atakiandaa maalumu kwa mchezo
huo. Mkwasa amesema kwamba anatarajia kuita
wachezaji 20 ambao atasafiri nao kwenda Nigeria
kwa ajili ya mchezo huo.
“Kutakuwa na mabadiliko kidogo katika kikosi
nitakachotangaza. Kwanza watakuwa wachezaji 20
badala ya 24, pili wachezaji ambao nitawachukua
ni tofauti tofauti maana wengine kwa sasa ni
majeruhi,” amesema Mkwasa.
Mchezo huo ni wa kukamilisha ratiba katika kundi
G baada ya Misri kukata tiketi ya kucheza Kombe
la Mataifa ya Afrika, fainali zitakazofanyika Gabon,
mwakani. Katika kundi hilo, Chad ilijitoa hivyo
kuathiri mbio za ushindani wa nafasi hiyo kwa
timu za Tanzania na Nigeria.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni