0

Licha ya kufungwa na Yanga katika mchezo wa
Agosti 13, timu ya Mo Bejaia ya Algeria ambayo
pia imelingana pointi na Medeama ya Ghana, lakini
kanuni za Kombe la Shirikisho zimeiwezesha timu
hiyo ya Algeria kusonga mbele katika hatua ya
nusu fainali.
Mo Bejaia imemaliza hatua ya robo fainali ikiwa na
pointi 8, sawa na Medeama lakini kwa kuwa katika
mchezo wa leo Jumanne uliozikutanisha timu hizo
kicha Mo Bejaia imeshinda kwa bao 1-0,
imefanikiwa kusonga mbele kwa kuwa kanuni
inasema mara baada ya timu kufungana pointi
kinachoangaliwa ni ‘head to head’ pindi
zilipokutana.
Wadau wengi walijua kuwa baada ya kulingana
pointi kitakachoangaliwa ni idadi ya mabao ya
kufunga au tofauti ya mabao ya kufungwa na
kufunga lakini kumbe sivyo.
Kwa kuwa zilipokutana awali, zilitosa suluhu ya
0-0, hivyo sasa Mo Bejaia imesonga mbele kwa
kusaidiwa na ushindi huo wa pili ilioupata leo.
TP Mazembe imeongoza kundi kwa kuwa na pointi
13, wakati Yanga imeshika mkia ikiwa na pointi
nne. Yanga iliifunga Mo Bejaia bao 1-0 jijini Dar es
Salaa wakati Mo Bejaia nayo iliifunga Yanga bao
1-0 katika mchezo wa kwanza.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top