Yanga imehitimisha rasmi michezo yake ya
kombe la shirikisho Afrika baada ya jioni ya leo
kukubali kichapo cha mabao 3-1 katika mchezo
mkali wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa
Stade de Frederic Kibassa Maliba,Lubumbashi.
Yanga SC ambayo ilimpoteza beki wake Vincent
Andrew Dante aliyelimwa kadi nyekundu dakika ya
30 ilijikuta ikiruhusu bao lililofungwa Jonathan
Bolingi dakika ya 28.
Rainford Kalaba aliiandikia TP Mazembe mabao
mengine mawili dakika za 55 na 65 kabla ya
Amissi Tambwe kuifungia Yanga SC bao la kufutia
machozi dakika ya 75.
Matokeo hayo yameifanya TP Mazembe ibaki
kileleni mwa msimamo wa kundi A baada ya
kufikisha alama 13.Yanga SC imebaki mkiani na
alama zake nne baada ya kushuka dimbani mara
sita.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni