0

Beki wa Crystal Place Damien Delaney amesema
kumsajili Christian Benteke 'si Lionel Messi' na
kwamba atahitaji kupokea usaidizi kutoka kwa
wachezaji wengine katika klabu hiyo..
Benteke mwenye umri wa miaka 25, alijiunga na
The Eagles kutoka Liverpool kwa thamani ya pauni
milioni 27.
'Hatumsajili Messi, ni (Benteke) mchezaji mzuri
lakini si mchezaji ambaye anaweza kupata mpira
na kubadilisha mchezo,'' Delaney aliambia gazeti
la Evening Stardard.
Benteke huenda akajiunga na Crystal Palace
wakikabiliana na Blackpool katika mechi ya EFL
Jumanne.
'Benteke analeta uhali kwenye timu, kama
mshambuliaji Connor Wickham. Ni wakati wetu
kuacha kuzungumza sana na kuangazia ushindi,"
Dalaney aliongezea.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top