0

Kocha mkuu mpya wa mabingwa wa Ujerumani
klabu ya Bayern Munich Muitaliano Carlo Ancellot
amemteua mwanae Davide Ancellot kuwa msaidizi
wake.
Bayern Munich wanaotumia uwanja wa Allianz
Arena walimtangaza jana Davide Ancellot mwenye
miaka 27 tu kuwa msaidizi wa kocha Carlo
Ancelltu katika kikosi cha Bayern Munich.
Davide ni mchezaji wa zamani wa timu ya vijana
ya AC Milan ambaye alishindwa kupata nafasi ya
kuichezea Milan katika Serie A na kuamua
kusomea ukocha.
Kijana huyo alikua na baba yake pia wakati Carlo
Ancellot alipoifundisha Real Madrid katika misimu
yake miwili ndani ya Santiago Bernabeu wakati
huo akiwa kama kocha wa viungo.


Katika picha ni Davide Ancellot kushoto akiwa na baba yake
katika benchi la ufundi la Bayern Munich



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top