Mlinda lango wa FC Barcelona Claudio Bravo
anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na klabu ya
Manchester City leo.
Bravo alitua jiji la Manchester jana Jumanne
mchana.
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola
amethibitisha juu ya klabu yake kuwa kwenye
hatua za mwisho kumsajili mlinda lango huyo wa
Kimataifa kutoka Chile.
"Siwezi kukataa kitu ambacho kila mtu
anakifahamu," amesema.
"Hata hivyo Bravo bado si mchezaji wetu sababu
hatujakamilisha usajili. Tutamtambulisha baada
taratibu zote kukamilika."
Kusajiliwa kwa Bravo kunaweka mashakani hatma
ya mlinda lango namba moja wa Uingereza Joe
Hart.
Hata hivyo inadaiwa mlinda lango huyo amegoma
kuondoka City, anataka kubaki Ciy kupigania nafasi
yake.
Sevilla na Borussia Dortmund zimeingia kwenye
harakati za kutaka kumsajili Hart.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni