0
Sitaki tena. ...Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kauli ya nyota wa filamu za kibongo Mirium Jolwa "Jini Kabula" ambaye amedai kuwa kwa sasa hataki kusikia mapenzi ya pesa na kama kuna mwanaume anayemtaka basi amfuate nyumbani na si kuitana baa..... Kabula alisema kuwa wanaume wengi wamekuwa na tabia ya kuitana baa huku wakihisi kuwa kila mwanamke ni mlevi kutokana na tabia ya baadhi ya wasanii ambao wamekuwa wakijirahisisha kwa kupewa pombe... "Siwezi kuvua nguo eti kwa sababu ya pombe wakati hata mwenyewe naweza kukaa baa na kunywa kwa pesa zangu. "Kama kuna mwanaume anataka kutulia na mimi si lazima tukae baa kwani kuna sehemu nzuri mnaweza kukaa na kuzungumza, nasema hivi ili wale wenye tabia hizo waache kabisa," alisema

Chapisha Maoni

 
Top