Ray C kugombea Ubunge 2015 ili kupigana na watu wanaoingiza madawa ya kulevya nchini
Makundi mengi ya vijana ndani ya
mtandao wa facebook yamekuwa na imani
kuwa msanii Rehema Chamila anaweza
kuwa mtetezi wao mkubwa endapo
ataamua kuingia kwenye siasa...
Vijana hao wanaamini kuwa Ray C kwa
sasa amepitia changamoto nyingi hivyo
wanaamini kama akipewa nafasi ya kuingia
bungeni inaweza kuwa chachu ya yeye
kupigana na watu wanaoingiza madawa ya
kulevya nchini na kuwaokoa vijana wengi
wanaopotea kutokana na matumizi ya
dawa hizo
"Ray C kwa nini asiingie tu kwenye siasa
na akatutetea kwenye mambo ambayo
hata yeye alikutana nayo hadi yakataka
kumtoa roho, tunaamini anaweza endapo
ataamua kufanya hivyo" alidai kijana
mmoja ndani ya mtandao wa facebook
Chapisha Maoni