Kijana afikishwa mahakamani jijini Mwanza kwa tuhuma za kukutwa akifanya mapenzi na mbuzi
MTU mmoja amefikishwa katika mahakama ya
wilaya ya Ukerewe, Mwanza kwa tuhuma za
kukutwa akifanya mapenzi na mbuzi.
Mtuhumiwa huyo, William Sebastian (21),
mkazi wa Kijiji cha Mlezi alisomewa mashtaka
hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya wilaya hiyo, Faustine Kishenyi.
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta
Samwel Onyango aliieleza mahakama hiyo
kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Juni
4 mwaka huu saa 9 alasiri huko Mlezi,
Ukerewe.
Katika hati ya mashitaka imeelezwa kuwa
mshitakiwa huyo alikutwa akitenda kosa hilo
katika banda la mbuzi nyumbani kwao na
mmoja wa wanafamilia.
Katika maelezo hayo, Onyango alisema
mwanafamilia huyo ambaye ni mwanafunzi wa
darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mlezi,
baada ya kushuhudia tukio hilo alikwenda
kutoa taarifa kwa baba yao, Maxmilian
Stephan aliyefika na kumkuta mtuhumiwa
akiendelea `kuhangaika’ na mbuzi huyo.
Akifafanua, alisema kosa hilo ni kinyume cha
sheria ya makosa la kujamiiana kifungu namba
K/F 154 (1) na (2) C sura ya 16 ya
marekebisho ya sheria ya mwaka 2002.
Mtuhumiwa amekana kutenda kosa hilo na
amerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini.
Chapisha Maoni