Kijana aliyedaiwa kupotea kwa Imani za kishirikina mkoani Mara apatikana akiwa katika hali ya kutisha huku mwili wake ukiwa umejaa tope
Kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambogo
wilayani Rorya mkoani Mara, ambaye
anadaiwa kupotea nyumbani kwa imani za
kishirikina hatimaye amepatikana huku akiwa
katika hali ya kutisha bila kujitambua na mwili
wake ukiwa umejaa tope jingi, tukio ambalo
limevuta mamia ya wananchi wa kijiji hicho.
Kijana huyo Kenedy oguko mwenye umri wa
miaka 22 amekutwa nje ya nyumba yao
asubuhi ya Juni 5 mwaka huu akiwa uchi wa
mnyama,ambapo baadhi ya mashuhuda wa
tukio hilo wamedai kuwa tangu kutoweka kwa
kijana huyo siku nne zilizopita,wamekuwa
wakimtafuta bila mafanikio huku wakihusisha
tukio hilo na imani za kishirikina.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya
ya Rorya Bw Samwel Kiboye,ambaye ni
miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo
amewaomba wananchi kuacha kulipiza visasi
kwa kuwasaka watu wanaotuhumiwa kwa
ushirikina bali watumie vyombo vya dola huku
mwenyekiti wa kijiji hicho akilaani vikali
vitendo hivyo vya ushirikina vinavyoendelea
kijijini hapo hatua ambayo amesema
imesabisha wananchi sasa kuishi kwa hofu
kubwa. Hata hivyo katika hali ya kushangaza wazee wa
jadi kijijini hapo waliagiza kila mwananchi
kupita mbele ya kijana huyo na kumpa mkono
kama njia moja wapo ya kuwezesha kupata
fahamu kitendo ambacho hata hivyo hakikuzaa
matunda.
Chapisha Maoni