Winga wa Real Madrid Gareth Bale amesaini
mkataba mpya wa miaka mitano na klabu yake
kwa mujibu wa ripoti
Nyota huyo wa kimataifa wa Wales, 27, alikuwa
mchezaji ghali zaidi duniani alipotimkia Bernabeu
2013, na tangia hapo ameiwezesha klabu yake
kutwaa mataji mawili Ligi ya Mabingwa.
Dili la awali la Bale lilikuwa linafikia kikomo 2019,
lakini Marca wameripoti kuwa amefikia
makubaliano mapya na klabu hiyo na atakuwa
mchezaji mwingine anayepokea mshahara mnono
Real Madrid sawa na Sergio Ramos na nyuma ya
Cristiano Ronaldo pekee.
Mkataba mpya utamfanya Bale adumu na
mabingwa hao wa Ulaya hadi 2021, pia Cristiano
Ronaldo inasemekana alishakubali mkataba mpya
lakini dili lake litathibitika Septemba.
Madrid wamekuwa kimya katika dirisha la usajili
msimu huu, jambo ambalo si kawaida yao, ujio
wa Alvaro Morata aliyerejea kutoka Juventus ndio
usajili pekee waliofanya majira ya joto.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni