Mabao mawili ya Mshambuliaji wa Ubelgiji, Michy
Batshuayi,yameipa Chelsea ushindi wa mabao 3-2
dhidi ya Bristal Rovers katika mchezo mkali wa
hatua ya nne ya michuano ya EFL (Kombe la Ligi)
uliochezwa usiku huu katika uwanja wa Stamford
Blidge.
Batshuayi alianza kuipa raha Chelsea baada ya
kuifungia bao la kuongoza dakika ya 29 ya
mchezo kabla ya dakika ya 31 Victor Moses
kuongeza bao la pili.Bao la tatu la Chelsea
limefungwa dakika ya 41 na Michy Batshuayi.
Mabao ya Bristal Rovers yamefungwa na Peter
Hartley dakika ya 34 ya mchezo pamoja na Ellis
Harrison aliyefunga bao la pili kwa mkwaju wa
penati na kufanya mchezo uishe kwa Chelsea
kutoka kifua mbele uwanjani kwa ushindi wa
mabao 3-2.
Katika mchezo mwingine Liverpool ikiwa ugenini
imechomoza na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya
Burton Albion shukrani kwa mabao ya Divock
Origi,Roberto Firmino,Tom Naylor na Daniel
Sturridge,aliyefunga mabao mawili.
Matokeo hayo yamezipeleka Chelsea na Liverpool
hatua ya tatu ya michuano ya EFL
Matokeo Mengine ya EFL yako kama Ifuatavyo
Crystal Palace 2 - 0 Blackpool
Blackburn Rovers 3 - 3 Crewe Alexandra
Burton Albion 0 - 5 Liverpool
Chelsea 3 - 2 Bristol Rovers Derby County 1 - 1
Carlisle United
Everton 4 - 0 Yeovil Town
Exeter City 1 - 3 Hull City
Luton Town 0 - 1 Leeds United
Millwall 1 - 2 Nottingham Forest
Newcastle United 2 - 0 Cheltenham Town
Northampton Town 2 - 2 West Bromwich Albion
Norwich City 6 - 1 Coventry City
Oxford United 2 - 4 Brighton & Hove Albion
Peterborough United 1 - 3 Swansea City
Preston North End 2 - 0 Oldham Athletic
Queens Park Rangers 2 - 1 Rochdale
Scunthorpe United 1 - 1 Bristol City
Stevenage 0 - 4 Stoke City
Watford 1 - 1 Gillingham
Wolverhampton Wanderers Cambridge United
Reading 1 - 1 Milton Keynes.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni