0

Baada ya kutekeleza ahadi ya mwanzo ya
kuipeleka Madagascar kwa ajili ya kambi ya
kuivaa Afrika Kusini ‘Amajimbos’, Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi amepanga kutekeleza ahadi yake
nyingine kwa kuipeleka timu ya taifa ya Tanzania
ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
‘Serengeti Boys’ kwenye kambi tulivu,
ikiwezekana nje ya nchi.
Rais Malinzi aliahidi na kutekeleza ahadi yake
kuipeleka Madagascar Serengeti Boys baada ya
kuitoa Shelisheli katika michuano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Madagascar,
mwakani. Kadhalika aliahidi kuipeleka timu hiyo
nje ya nchi ambayo hata hivyo haijateuliwa baada
ya kuindoa Afrika Kusini. Ameahidi kambi hiyo
itaanza Septemba mosi, mwaka huuu.
Serengeti Boys ilipiga kambi Hosteli za TFF, zilizo
Karume kwa wiki moja kabla ya kuhamia Hoteli ya
Urban Rose, katikati ya jiji la Dar es Salaam
ambako ilivunjwa kwa muda jana Agosti 22, 2016
ambako vijana wamekwenda makwao kusalimia
ndugu zao na itaitwa mwishoni mwa mwezi huu
kwa ajili ya maandalizi ya kambi ya nje ya nchi.
Serengeti Boys imebakiwa na mtihani mmoja
kufuzu kucheza fainali hizo kwa kucheza na
Congo – Brazaville na mchezo wa kwanza
utafanyika Dar es Salaam, Septemba 18, 2016
kabla ya kurudiana Septemba 30, 2016, Oktoba 1
au Oktoba 2, 2016.
TFF imejipanga kwa ajili ya kambi hiyo, na
kinachosubiriwa kwa sasa ni mapendekezo ya
makocha ili shirikisho itekeleze hatua hiyo ya
kambi ya utulivu.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime
maarufu kama Mchawi Mweusi amesema kwamba
anaamini kuwa mchezo ujao utakuwa mgumu kwa
kuwa kila timu nitajipanga kuvuka ili kucheza
fainali hizo.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top