0

KLABU ya Watford imeendelea na harakati za
kukiimarisha kikosi chake hii ni baada ya jioni ya
leo kutangaza kukamilisha usajili wa mlinzi wa
kulia wa Kidachi Daryl Janmaat kutoka Newcastle
United kwa ada ya £7m.
Janmaat,27,amesaini mkataba wa miaka minne wa
kuitumikia Watford na anatarajiwa kuanza
kuichezea klabu hiyo Jumamosi ya wiki hii pale
itakaposhuka dimbani kuvaana na Arsenal katika
muendelezo wa michezo ya ligi kuu Uingereza.
Janmaat alijiunga na Newcastle United mwaka
2014 kwa ada ya £5m akitokea Feyenoord ya
nyumani kwao Uholanzi na kufanikiwa kuichezea
michezo 78 akifunga mabao manne klabu ya klabu
hiyo kushuka daraja msimu uliopita.
Janmaat anakuwa mchezaji wa nane kujiunga na
Watford msimu huu baada ya Jerome Sinclair,
Christian Kabasele, Isaac Success, Juan Camilo
Zuniga, Brice Dja Djedje, Younes Kaboul na
Roberto Pereyra.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top