Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger,ameonyesha
nia ya kutaka kuwauzia Real Madrid nyota wake
raia wa Chile,Alexis Sanchez,katika kipindi hiki cha
usajili ama kile cha mwezi Januari lakini kwa sharti
la yeye kupewa wachezaji wawili.
Kwa mujibu wa gazeti la Don Balon ni kwamba
wachezaji wanaotakiwa na kocha Arsene Wenger ni
Mcolombia James Rodriguez pamoja na Mhispania
Alvaro Morata.
Alvaro Morata
Don Balon limeendelea kupasha kuwa Arsenal
imesema kuwa katika dili lolote lile la kumtaka
Sanchez lazima Real Madrid imjumuishe
mshambuliaji wake Alvaro Morata,vinginevyo
hakutafanyika biashara ya aina yoyote ile.
Wakati huohuo taarifa kutoka nchini Italia zinasema
Inter Milan nayo imejitosa kumwania Sanchez na
tayari imeshaandaa ofa ya €80m ili kuhakikisha
inamsajili katika kipindi hiki cha usajili barani
Ulaya.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni