Simba na Yanga zimegawana pointi baada ya sare ya bilabkufungana jioni ya leo Uwanja wa, Taifa, Dar es Salaam huku kipa chipukizi Peter Manyika akiibuka shujaa kwa kuokoa michomo kadhaa ya hatari.
Kipa huyo wa tatu, Manyika alidaka mechi hiyo ya watani leo kwa sababu kipa wa kwanza Ivo Mapunda na wa pili, Hussein sharrif ‘Casillas’ wote ni majeruhi na Yanga SC walikuwa wanaamini watashinda kwa urahisi dogo huyo akiwa langoni.
Kwa ujumla, makipa wa timu zote mbili, Peter Manyika wa Simba SC na Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga SC walifanya kazi zao vizuri leo.
Dida alikuwa wa kwanza kuinusuru timu yake kufungwa mapema dakika ya sita, baada ya kudaka shuti la Emmanuel Okwi aliyepiga ndani ya boksi.
Yanga walijibu shambulizi hilo dakika hiyo hiyo, baada ya Mbrazil, Genilson Santana Santos ‘Jaja’ kuiunganishia nje krosi maridadi ya Oscar Joshua.
Manyika mdogo naye akadaka shuti la
Mbrazil, Andrey Coutinho dakika ya 13 na kuwakatisha tamaa mashabiki wa Yanga SC waliodhani yeye ni mwepesi kufunga.
Mshambuliaji Mganda, Okwi tena
aliunganishia nje kwa kichwa krosi nzuri ya William Lucian ‘Gallas’ akiwa kwenye nafasi nzuri na kubaki amejishika kichwa kujilaumu.
Kipindi cha pili, Simba SC ndiyo walioanza kupeleka mashambulizi na dakika ya 46 tu, Elias Maguri alipiga juu ya lango baada ya kupewa pasi nzuri na ‘Gallas’.
Jaja tena aliikosesha Yanga bao dakika ya 73 baada ya kuunganishia juu ya lango krosi maridadi ya Simon Msuva aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima. Manyika akaokoa tena shuti kali la Jaja dakika
ya 76 na kuzidi kuwakatisha tamaa Yanga SC na kocha wao, Mbrazil Marcio Maximo.
Matokeo hayo, yanaifanya Yanga SC itimize pointi saba baada ya kucheza mechi nne, ikishinda mbili, kufungwa moja na sare moja, wakati Simba imeendelea kuokota pointi moja
moja, kwa sare ya nne mfululizo.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Peter Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Jonas kude/Pierre Kwizera dk60, Emmanuel Okwi,
Said Ndemla/Shaaban Kisiga dk38, Elias
Maguri, Amri Kiemba/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk81 na Haroun Chanongo.
Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/ Salum Telela dk70, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Mrisho Ngassa, Hassan Dilunga, Genilson Santana Santos ‘Jaja’/Hamisi Kiiza
dk82, Haruna Niyonzima na Andrey Coutinho.
Chapisha Maoni