0

TOTO Africans ya Mwanza imeuanza vyema msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) baada ya
jioni ya leo kuishushia Mwadui FC kichapo cha bao
1-0 katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja
wa CCM Kirumba,Mwanza.
Bao la ushindi katika mchezo huo pekee wa ligi
kuu Jumatano ya leo limefungwa dakika ya 36 na
Mshambuliaji Waziri Junior Shentembo.
Hii ni mara ya tatu kwa Toto Africans kuitambia
Mwadui FC katika michezo ya ufunguzi wa pazia la
ligi kuu bara.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top