Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans Pluijm,
amefichua kilichofanywa na wachezaji wake mpaka
ikafanya vibaya kwenye michuano ya kimataifa,
huku akisema kadi walizopewa Donald Ngoma na
Thabani Kamusoko zilichangia.
Yanga ambayo jana Jumanne ilikamilisha ratiba
yake ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kucheza
dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, haikuwa na
msimu mzuri kwenye michuano hiyo hali
iliyowashusha morali ya mashabiki wake.
Kabla ya mchezo wao wa jana, Yanga ilikuwa tayari
imeshacheza mechi tano dhidi ya MO Bejaia,
Medeama na TP Mazembe na kufungwa tatu, sare
moja na kushinda moja, ikikusanya pointi nne.
“Ni lazima tulipaswa kupata ushindi kwenye mechi
za nyumbani, pia tulifanya makosa mengi kwenye
safu yetu ya ulinzi na hiyo ndiyo ilitufanya
tufungwe mabao ambayo mengine ni ya kizembe.
“Kiukweli mechi za nyumbani ni lazima ushinde,
usipofanya hivyo kwako unadhani utawezaje
ugenini, yote kwa yote huu ni mpira, tunakubali
matokeo ya aina yoyote yale.
Katika hatua nyingine, Pluijm alisema kitendo cha
kuwakosa mara kwa mara wachezaji wake ambao
wengi walikuwa ni watovu wa nidhamu na
kulazimika kukosa mechi kutokana na kutumikia
kadi za njano na nyekundu kilichangia hali hiyo.
Ikumbukwe kuwa, katika mechi hizo zote mpaka
Yanga inamaliza mchezo wake wa jana ambapo
ilifungwa mabao 3-1 na TP Mazembe, iliwakosa
Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Amissi
Tambwe, Haruna Niyonzima, Vincent Bossou na
Kelvin Yondani, ambao walikuwa na kadi mbili za
njano huku Haji Mwinyi, Nadir Haroub ‘Cannavaro’
wakikosa baadhi ya mechi kwa kuwa na kadi
nyekundu.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni