0

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeweka bayana
kuwa, lipo kwenye mpango wa kuwakabidhi kombe
jipya la Ngao ya Jamii timu ya Azam kutokana na
kukabidhiwa kombe ambalo halikuwa lenyewe.
Azam waliichapa Yanga kwa penalti 4-1 katika
mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kumaliza
dakika tisini kwa sare ya mabao 2-2, kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameliambia
Championi Jumatano kuwa, waliwapa Azam ngao
ambayo siyo yenyewe kutokana na kuchelewa
kukamilika kwa utengenezwaji wa ngao halali
ambayo walitakiwa kupewa.
“Lile kombe ambalo tuliwapa Azam siku ile
walipocheza na Yanga kwenye Ngao ya Jamii
halikuwa lenyewe, bali tulilitoa kwa ajili ya kuziba
nafasi ya kombe halisi ambalo lilichelewa kuja
kutokana na kutokamilika mpaka inafika siku ile,
hivyo tukaona siyo vizuri bingwa akiondoka
mikono mitupu.
“Tumepanga kuwabadilishia na kuwapa kombe lao
halisi ambalo walistahili kupewa ambalo hili
litakuwa na thamani halisi na mwonekano tofauti
kabisa na lile ambalo tulilitoa awali,” alisema
Lucas.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top