Kocha Jose Mourinho amejitetea baada ya maamuzi yake ya kumtosa Bastian
Schweinsteiger ambaye ni kiungo mkongwe na kusisitiza kuwa anataka kufanya kazi na wachezaji 23!
Mourinho amekuwa kikaangoni baada ya kumlazimisha Mjerumani huyo ambaye
ni mshindi wa Kombe la Dunia kufanya mazoezi na kikosi cha chini ya miaka 23! Kocha huyo mpya wa United amejitetea na kudai kuwa alichokifanya
ni sawa na kwamba anapaswa kupiga panga kikosi chake ili kupisha wachezaji wapya aliowasajili.
“Ninapaswa kufanya maamuzi yangu. Ni hivyo tu. Kilichofanyika ndicho
kinachofanyika kwenye kila klabu duniani, ni kocha ndiye anayeamua juu ya kikosi chake!”
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni