Mechi ya mwisho ya Liverpool katika ziara yake
nchini Marekani imemalizika kwa kichapo cha bao
2-1 toka kwa AS Roma ya Italia.
Roma ilianza kupata bao dakika ya 29 likifungwa
na Edin Dzeko baada ya kazi nzuri ya Kevin
Strootman kisha Kinda Oluwaseyi Ojo
akaisawazishia Liverpool dakika moja kabla ya
mapumziko.
Mshambuliaji Mohamed Salah akamalizia ushindi
kwa Roma akifunga bao safi dakika ya 63 akitumia
makosa ya kipa wa Liverpool Simon Mignolet.
Liverpool sasa inarejea England tayari kwaajili ya
msimu mpya wa ligi ambapo itafungua dimba
dhidi ya Arsenal.
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni