Uongozi wa Simba kumkaribisha kwenye kikao
cha kamati ya utendaji lakini baadaye umeandika
barua pia kuomba fedha kwa ajili ya usajili
Baada ya jana uongozi wa Simba kukumbwa na
wakati mgumu mbele ya wanachama wa klabu
hiyo kutokana na kuchelewesha mpango wa
mabadiliko wa timu hiyo kuchukuliwa na Bilionea
Mohamed Dewji ‘MO’ hatimaye viongozi hao leo
wamemuandikia barua mfanyabiashara huyo na
kumktaka kuhudhuria kikao maluum cha kamati
ya utendaji ya klabu hiyo, ili kueleza dhamira
yake ya kutaka kuwekeza kiasi cha shilingi
billioni 20.
Katibu mkuu wa klabu ya Simba Patrick
Kahemele, ameiambia Goal , wanataka kusikia
maneno hayo kutoka kwake mwenyewe na siyo
kupitia kwenye vyombo vya habari ili
awathibitishie kile ambacho amekusudia kuifanyia
klabu yao.
Katika barua hiyo “Mo” ameombwa kukutana na
kamati ya utendaji ya klabu ya Simba Agust 15
mwaka huu.
Hiyo hapo chini ndiyo barua iliyoandikwa na
uongozi wa Simba kwenda kwa ‘MO’
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni