Timu ya Rubin Kazan imemsajili kiungo Alex Song
bure kwa mkataba wa mitatu kutoka kwa miamba
wa Hispania Barcelona. Song aliitumika West Ham
msimu uliopita kwa mkopo baada ya kukosa nafasi
ya kudumu katika kikosi cha Barcelona.
Klabu ya Southampton imemsajili golikipa Alex
McCarthy kwa mkataba wa miaka mitatu toka timu
ya Crystal Palace. McCarthy, alicheza michezo
saba msimu uliopita akiwa na klabu yake ya
Crystal Palace huu ni usajili wa tatu wa Watakatifu
hao wa Southampton baada ya kuwasajili Nathan
Redmond Pierre-Emile Hojbjerg.
Nae beki Steven Taylor amejiunga na timu ya
Portland Timbers, inayoshiriki ligi ya kuu ya
Marekani akitokea Newcastle United. Beki amekaa
kwenye klabu ya Newcastle kwa muda wa 21 toka
akiwa mdogo, na amecheza michezo 268.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni