0

KIPA wa Platinum Stars ya Afrika Kusini,Mbongeni
Mzimela (Pichani) usiku wa kuamkia leo Jumapili
ameibuka shujaa baada ya kufunga mabao mawili
katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Vipers SC ya
Uganda katika mchezo wa marudiano wa hatua za
awali wa kombe la shirikisho barani Afrika.
Katika mchezo huo uliochezwa huko Royal
Bafokeng-Rustenburg,Afrika Kusini,imeshuhudiwa
Mzimela akiifungia Platinum Stars mabao hayo
yote kwa mikwaju ya penati iliyopatikana katika
kipindi cha kwanza na cha pili.
Bao jingine la Platinum Stars iliyolazimika
kumaliza mchezo ikiwa pungufu baada ya Robert
Ng'ambi kutolewa uwanjani kwa kadi mbili za
njano limefungwa na Ndumiso Mabena huku lile la
Vipers SC likufungwa na Milton Karisa.
Kwa ushindi huo sasa Platinum Stars inasonga
hatua inayofuata kwa ushindi wa jumla ya mabao
3-2.Ikimbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa
jijini Kampala,wenyeji Vipers SC walishinda bao
1-0.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top