0

MABINGWA watetezi,Mamelodi Sundowns
wameungana na Zanaco FC ya Zambia kutinga
hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa
Afrika baada ya jioni hii kutoka sare ya kufungana
bao 1-1 na KCCA ya Uganda kwenye mchezo
mkali wa marudiano wa hatua ya mtoano
uliochezwa hukoPhilip Omondi
Stadium,Nambore,Uganda.
Bao lililowapeleka Mamelodi Sundowns kwenye
hatua ya makundi limefunga na mshambuliaji wake
Mliberia,Antony Laffor katika dakika ya 80.Kabla ya
bao hilo KCCA walikuwa mbele kwa bao moja
lililofungwa mapema katika dakika ya 30 ya kipindi
cha kwanza na Geoffrey Serunkuma akiunganisha
krosi safi ya Brian Majwega.
Kwa sare hiyo sasa ina maana kwamba Mamelodi
Sundowns imefuzu hatua ya makundi kwa ushindi
wa jumla wa mabao 3-2 baada ya kushinda mabao
2-1 katika mchezo wa awali uliochezwa Jumamosi
iliyopita kwenye uwanja wa Moses Moripe huko
Pretoria, Afrika Kusini.
Katika mchezo mwingine,Zanaco FC ikiwa
nyumbani Lusaka imefuzu hatua ya makundi baada
ya kutoka sare ya bila kufungana.Katika mchezo
wa awali uliochezwa Dar Es Salaam timu hizo
zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.
Vikosi
KCCA : Ocan, Okot, Kavuma, Awany,
Ochaya,Mutyaba, Kirabira, Mucureezi,
Okello,Majwega, Serukuuma
Sundowns: Sandilands, Ngcongca (Laffor
46′),Nascimento, Arendse, Langerman,
Kekana,Mabunda (Mashaba 71′), Morena,
Zwane,Zakri, Tau



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top