0

SIKU chache baada ya kupanda ligi kuu bara,
Singida United imejinasibu kuwa imejipanga kuja
kuleta mabadiliko ya kweli kwenye ligi hiyo kubwa
zaidi nchini Tanzania.
Katibu mkuu wa timu hiyo, Abdul Sima amesema
uongozi wa Singida United umepanga kuiendesha
timu hiyo kisasa zaidi kwa kuifanya kuwa kampuni
ambapo mashabiki watapata fursa ya kumiliki hisa
badala ya kadi za uanachama ambazo hazina tija
sana.
Wakati huohuo Sima ameongeza kuwa Singida
United haitaacha mchezaji yoyote yule kutoka
kwenye kikosi kilichoirejesha timu hiyo ligi kuu
bara labda kama mchezaji ataamua kuondoka
mwenyewe.
Pia Sima amesema makocha Jumanne Charles na
Fred Minziro ambao wameipandisha daraja Singida
United wataendelea na vibarua vyao licha ya timu
hiyo juzi Ijumaa kumwajiri Mholanzi Hans Van
Pluijm kuwa kocha wake mkuu.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top