0

Ivan Rakitic amemtaja mchezaji wa Real Madrid
mwenye uwezo wa kucheza kwenye kikosi cha
Barcelona
Kiungo wa Barcelona Ivan Rakitic amemtaja Luka
Modric kama moja ya wachezaji Real Madrid
ambao wanaweza kucheza Barcelona. Katika
mahojiano na gazeti la Marca alisema, “Ni mtu
ninayemheshimu sana; naam, anaweza kucheza
Barcelona kwa mimi nionavyo kwa sababu yumo
kwenye orodha ya wachezaji bora watatu katika
nafasi yake.”
“Nafurahia sana kucheza naye na kwa heshima
aliyo nayo kwa kila mmoja, tunaona tofauti
kwenye kikosi cha Real Madrid anapokuwepo na
anapokosekana kikosini,” aliendelea.
Ivan Rakitic na Luka Modric wanacheza wote
timu moja ya taifa Croatia. Kama Ivan Rakitic
anavyoeleza, “Ni rafiki yake sana na
anamuheshimu mno kama mchezaji mwenzake
na rafiki. Tumekuwa pamoja kwa muda wa
takribani miaka 10 kwenye timu ya taifa. Lakini ni
rafiki nje ya soka pia, na tunapoongea hatuongei
sana kuhusu soka; ni zaidi ya familia na mambo
mengine.”
Kwa hiyo uwezo wake mkubwa uwanjani
unaweza kumfanya apate namba kwenye kikosi
cha Barcelona, licha ya vipaji vingi kwenye timu
yao, hasa katika sehemu ya kiungo.
Luka Modric ameleta mapinduzi tangu alipotua
Real Madrid, kwa uwezo wake wa kupiga pasi na
pia namna anavyotembea na mpira. Kama Ivan
alivyosema, Real ni timu tofauti kabisa inapokuwa
na Modric na anapokosekana.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top