0

Hans Poppe amesema wakati wanamsajili
mchezaji huyo walitambua ubora wake na hata
alipokuwa anafanya vibaya waliendelea
kumvumilia wakiamini anaweza
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya
Yanga Zacharia Hans Poppe, amesema ubingwa
wao wa msimu huu utatokana na mabao ya
mshambuliaji wao Laudit Mavugo.
Hans Poppe ameiambia Goal, kiwango cha
Mavugo kimeonyesha namna gani walivyokuwa
na subira hata kufanikiwa kurudi kwenye kiwango
chake baada ya kuanza vibaya.
“Mavugo ndiye atakayetupa ubingwa msimu huu
kwa sababu ni mchezaji ambaye amebezwa sana
lakini sasa ameanza kutulipa zile garama tulizo
msajilia,” amesema Hans Poppe.
Kiongozi huyo amesema wakati wanamsajili
mchezaji huyo walitambua ubora wake na hata
alipokuwa anafanya vibaya waliendelea
kumvumilia wakiamini anaweza kufanya vizuri.
Amesema kama mshambuliaji huyo angeanza
kuonyesha uwezo wake tangu mwanzoni mwa
msimu basi timu yao ingekuwa mbali na hata
yeye binfasi angekuwa ndiyo kinara wa mabao
kwenye ligi.
“Mavugo anaonyesha thamani yake na haya
ndiyo matunda ya uvumilivu, kwake tunaamini
yeye ndiyo atatubeba kutokana na kiwango chake
na msaada wake kwenye timu,”amesema Hans
Poppe.
Aidha kiongozi huyo amesema endapo timu yao
itafanikiwa kuwa mabingwa wa ligi ya Vodacom
msimu huu anaamini mshambuliaji huyo
wanaweza kumkosa kutokana na kuonekana na
timu nyingine wakati watakapo shiriki michuano
ya kimataifa.
Mavugo aliyejiunga na Simba mwanzoni mwa
msimu huu, ameifungia Simba mabao 7 kwenye
ligi na kasi yake imekuwa ni ya kutisha hasa
baada ya kuanza kwa mzunguko wa pili.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top