Jamie Redknapp ameponda kikosi cha wachezaji
wa Arsenal baada ya kupigwa 3-1 na West Brom
katika mechi ya Ligi Jumamosi
Craig Dawson aliwapa West Brom goli la
kuongoza lakini Alexis Sanchez alifunga dakika
tatu baadaye na kufanya matokeo kuwa moja
moja hadi mapumziko.
Lakini West Brom walikuwa kikosi bora zaidi
kipindi cha pili na waliadhibu Gunners kwa
ukabaji wao mbovu.
Hal Robson-Kanu alifunga goli lake la kwanza
nyumbani kabla ya Dawson kufunga goli lake la
pili la mchezo kuipatia pointi tatu timu yake.
“Kwa kiwango kama kile huwa mameneja
wanafukuzwa,” Redknapp alikiambia Sky Sports .
“Arsenal walicheza shaghalabaghala. Sijawahi
kuona timu kubwa inayojua kwamba inacheza
dhidi ya timu yenye uwezo mkubwa wa
kutengeneza nafasi ikikaba kama vile.
“Kwa hakika yupo mtu aliyewaambia kabla ya
mechi wawe makini, McAuley, Dawson, ni watu
wenye uwezo mkubwa. Wanahitajika viongozi
kwenye chumba cha kubadilishia nguo, lazima
awepo mhamasishaji.
“Sijawahi kuona ukabaji wa kibwege kama ule.
Nawaonea huruma mashabiki wa Arsenal
walioendesha magari yao kwenda uwanjani.
Nilitaraji wangecheza vizuri lakini walifanya vibaya
sana.
“Arsene Wenger amepigwa fimbo nyingi, nadhani
alikuwa kwenye chumba cha kubadili nguo
akiwaambia wachezaji anachijisikia kwa sababu
wamemwangusha na klabu pia.”
Arsenal pia imepata pigo Jumamosi baada ya
Petr Cech, Alexis Sanchez kuumia.
Nafasi ya Cech ilichukuliwa na David Ospina
baada ya kupata majeraha ya misuli ya mguu na
Alexis Sanchez naye aliumia pia.
Arsenal wanashika nafasi ya tano na wanaweza
kushushwa na Manchester United kesho ikiwa
wataifunga Middlesbrough.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni