ishara ya kubakia kwake Klabuni hapo baada
kuzungumzia mipango yao ya kabla Msimu Mpya
wa 2017/18 kuanza.
Wenger, ambae Mkataba wake na Arsenal
unamalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari
upo Mezani Mkataba Mpya wa Miaka Miwili,
amekataa kutoboa kama ataendelea na Arsenal au
atang’oka huku kukiwa na presha kutoka Kundi la
Mashabiki wakitaka aondoke.
Mkataba wa Wenger, mwenye Miaka 67 na
ambaye yuko Arsenal kwa Miaka 20, unaisha Juni
lakini ametoa fununu za mipango yake kwa ajili ya
Msimu Mpya unaoanza Agosti.
Wenger ameeleza: “Ninayo Mipango. Hiyo ndio
kazi yangu kupanga.”
Alipobanwa nani atatangaza kama atabaki Arsenal,
Wenger alijibu: “Klabu. Sina la kuongeza hapo.
Siwezi kusema zaidi na nlichosema awali!”
Hivi karibuni Wenger alitamka kuwa ashaamua
kuhusu kubaki au kuondoka Arsenal na Watu
wasubiri tamko tu.
Hivi sasa Arsenal wapo Nafasi ya 5 kwenye EPL,
Ligi Kuu England, na pia Nusu Fainali ya FA CUP
ambako watacheza na Man City kwenye Nusu
Fainali.
Chapisha Maoni