0
Baada ya tetesi nyingi kuhusu mustakabali wa Kingsley Coman, Bayern wamempa mkataba kudumu kubaki Ujerumani hadi 2020 Bayern Munich imethibitisha usajili wa Kingsley
Coman kwa mkataba wa kudumu kutoka
Juventus.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akitumika kwa mkopo Bayern tangu mwanzo wa kampeni za 2015-16, akiwa na umri
wa miaka 20 na kucheza mechi 35 msimuwao wa kwanza Allianz Arena.
Coman amefunga mara mbili tu katika mechi 17 Bundesliga msimu huu, na imedaiwa kuwa Bayern hawakuwa na mpango wa kubaki na mchezaji huyo aliyekuwa akihusishwa na tetesi
za kujiunga na Arsenal na Chelsea.
Tetesi hizo sasa zimefutiliwa mbali, hata hivyo, baada ya miamba hao wa Ujerumani kuthibitisha kwamba Coman amesaini mkataba wa kudumu
hadi Juni 2020.
Mkurugenzi mtendaji wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge amesema: "Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa. Tumeshawishika kwamba
atakuwa na msaada mkubwa miaka ijayo."
Coman amecheza mechi sita kwenye timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya Ulaya 2016.

Chapisha Maoni

 
Top