0
Klabu ya Yanga imetangaza Mapato
yaliyopatikana ndani ya Siku nne toka
watangaze namba Maalumu kwa
Wanachama na Mashabiki ili kuweza
kuichangia klabu hiyo.
Makusanyo haya yanafanyika kupitia
mitandao ya Mpesa , Tigo Pesa na
Airtel Money.
Kwa taarifa ya klabu kwa wanachama
wake imesema mpaka sasa mwitikio
ni mzuri na wamewashukuru sana
wanachama wao kwa moyo mkubwa
kwa timu yao.
Ripoti yao inaanzia siku ya kwanza ya
tarehe 24 April 2017 saa saba mchana
walipozindua harambee hiyo mpaka
tarehe 27 April 2017 saa 7 mchana.
Makusanyo
 24 April 2017 walipokea miamala 642
na jumla ya makusanyo ikawa
2,184,911, 25 April 2017 walipokea
Miamala 1181 na jumla ya makusanyo
ikawa Tsh 4, 248,751.
26 April 2017 walipokea Miamala 625
na jumla ya makusanyo ikawa Tsh
2,296,966, 27 April 2017 walipokea
Miamala 290 na jumla ya makusanyo
ikawa Tsh 866,795.
Jumla.
Jumla ya Miamala waliyopokea ni
2738 na kukusanya kiasi cha fedha
cha Tsh milions 9,597,423.
Uongozi Umesisitiza kuwa fedha hizo
zitatumika kwa malengo
yaliyokusudiwa baada ya kukusanywa,
Lakini wakatoa angalizo kwa
Wanachama kuwa wachangiaji
wamekuwa wakishuka Idadi toka siku
ya kwanza, hivyo kwa Tafiti zao
imeonesha kuwa hamasa inazidi
kushuka siku hadi siku.
Shukrani.
Aidha Katibu Mkuu Charles Boniface
Mkwasa kwa niaba ya uongozi
amewashukuru wanayanga na
kuwaomba ripoti hiyo iwe chachu ya
kuchangia zaidi ili juma lijalo taarifa
iwe zaidi ya hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top