Shirikisho Yanga SC wameelekea
Mkoani Geita ambapo wataweka
kambi ya siku mbili kwa ajili ya
kujiandaa kwa mchezo wa nusu fainali
ya michuano ya Kombe La Shirikisho
'Azam Sports Federation' mchezo
utakaofanyika Jumapili kwenye uwanja
wa CCM Kirumba.
Timu hiyo ambayo iliwasili Jijini
Mwanza Alhamisi Jioni na
kupokelewa kwa shangwe na
mashabiki iliondoka moja kwa moja
na kuelekea Geita ambapo itaendelea
na programmu ya mazoezi yake.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya
timu hiyo kocha msaidizi wa Yanga
Juma Mwambusi amesema
wamefanya maandalizi mazuri na
wako tayari kuwavaa Mbao.
Maandalizi
-Tumefanya maandalizi mazuri,timu
iko vizuri na wachezaji wana ari ya
kushinda, tunajua Mbao ni timu
ngumu lakini tutajitahidi na
kuhakikisha tunapata
ushindi,tumeyafanyia kazi mapungufu
yetu na tunaimani tutashinda tunajua
ni timu nugumu lakini tunaahidi
ushindi" Alisema.
Milioni 50
Yanga watakutana na Mbao katika
Nusu Fainali ya pili nao Simba
wakiwavaa Azam katika nusu fainali ya
kwanza itakayofanyika Jumamosi
kwenye uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mshindi wa fainali hizo atapokea
shilingi milioni 50 pamoja na kupata
nafasi kuiwakilisha nchi katika
michuano ya kimataifa ya Kombe La
Shirikisho Barani Mwakani.
Chapisha Maoni