0
Siku chache baada ya wapenzi na
mashabiki wa soka Mjini Singida
kuelezea hofu yao juu ya kutokamilika
kwa Uwanja wa Namfua na kutumiwa
na Singida United kwa michuno ya ligi
kuu Tanzania bara, Serikali imeingilia
kati na kuhakikisha kuwa shughuli za
ukarabati zinaanza kufanyika.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt
Rehema Nchimbi amesema shughuli
za ukarabati huo sasa zitafanyika
usiku na mchana ili kuhakikisha kuwa
uwanja huo wa Chama Cha Mapinduzi
unakamilika kabla ya Agosti mwaka
huu.
-Kwa gharama yoyote ile, na hata
ikilazimika kufanya kazi usiku na
Mchana ni lazima uwanja huu
ukamilike mapema na uweze
kutumiwa na Singida United kama
uwanja wao wa Nyumbani msimu ujao
wa Ligi kuu” Nchimbi alisema.
Uzembe umefanyika.
Msimamizi huyo wa Shughuli zote za
kiserikali Mkoani Singida, amekiri
kwamba kuna uzembe umefanyika
katika kuukarabati uwanja huo, lakini
amesema si wakati wa kumtafuta nani
amekosea bali kujitahidi ili Singida
United wautumie uwanja huo Kuanzia
Agosti mwaka huu.
-Kuna uzembe umefanyika lazima
tukiri, lakini huu si wakati wa kutafuta
nani amefanya amekosea, bali kutafuta
namna ya pamoja ya kuweza
kuukamilisha mapema na Uwanja huu
uweze kutumika Msimu ujao na
Singida United’ Aliongeza Nchimbi.
Kila mdau.
Katika Upande Mwingine Dkt Rehema
Nchimbi ametoa wito kwa kila mdau
wa michezo mkoa humo kutimiza
wajibu wake ili uwanja huo uweze
kukamilika kwa wakati, na kuanza
kutumika kuanzia mwezi Agosti
mwaka huu.
Singida United iliyoshuka daraja miaka
15 iliyopita, imebahatika kupanda tena
msimu huu na inatarajia kutumia
Namfua kama Uwanja wake wa
nyumbani kwa michuano ya ligi kuu
Tanzania bara.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top