wa Miaka 17 'Serengeti Boys',
imemaliza kambi yake Salama Mjini
Rabat, nchini Morocco na imeelekea
Yaoundé Cameroon ambapo
wamepangiwa michezo ya kirafiki
dhidi ya timu ya vijana ya Cameroon.
Timu hiyo ambayo ilikuwa imepiga
kambi ya takriban mwezi mmoja
nchini Morocco imeonyesha
kuimarisha kiwango chake pakubwa
hatua inayonekana kumridhisha Kocha
Mkuu wa Timu hiyo Bakari Shime
'Mchawi Mweusi' ambaye amekiri
Timu hiyo kuonyesha mafanikio
makubwa na ana imani watafanya
vizuri katika fainali ya Michuano ya
Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya
umri wa miaka 17 yatakayofanyika
nchini Gabon.
Msafara wa Serengeti Boys
unaongozwa na Mkurugenzi wa soka
la vijana la Shirikisho la Soka Nchini
TFF, Ayubu Nyenzi unatarajiwa kufika
Yaounde saa 10.35 Alfajiri ya Ijumaa.
Cameroon
Wakiwa Mjini Yaounde, Serengeti Boys
watacheza michezo miwili ya kirafiki
na Timu ya Vijana ya Cameroon,
mchezo wa kwanza utafanyika
Jumamosi huku mchezo wa
marudiano ukifanyika siku ya
Jumanne.
Mara baada ya Kambi hiyo ya
Takribani Juma moja, Serengeti Boys
wataelekea Gabon Mei 7 kwa
matayarisho ya fainali hizo ambapo
wamepangwa kundi B pamoja na timu
za Taifa za Vijana za Angola, Niger na
Ethiopia.
Chapisha Maoni