0
Joshua ambaye mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo unamalizika mwishoni mwa msimu huu na hajui mstakabali wake kutokana na viongozi
kuwa kimya Beki wa kushoto wa Yanga Oscar Joshua, amesema mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo unamalizika mwishoni mwa msimu huu na hajui
mstakabali wake kutokana na viongozi wa timu hiyo kukaa kimya.
Joshua ni mmoja ya wacheza wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu, lakini amefungua milango kwa timu nyingine zitakazo
muhitaji endapo Yanga hawatamuhitaji tena kuendelea naye msimu ujao.
Joshua ameiambia Goal, kutokana na hali hiyo ameamua kuzikaribisha timu zitakazo muhitaji, wakiwemo wapinzani wao Simba, endapo
watavutiwa na huduma yake.
“Kufungua milango kwa timu nyingine,
haimaanishi kuwa siipendi Yanga, bado
ningependa kubaki hapa ila ukimya ndiyo unao nichanganya ukizingatia ligi inakwenda mwishonii a naona kimya kimezidi kutawala binfasi yangu
pamoja na kuifanyia Yanga mambo makubwa lakini sijui kama nitakuwemo kwenye mipango ya kocha msimu ujao,”amesema Joshua.
Mlinzi aliyetua Yanga misimu minne iliyopita akitokea Ruvu Shooting ya Pwani amesema kitu kingine kinachomfanya kutaka kuondoka kwenye timu hiyo ni kukosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza na kujikuta muda mwingi akiumalizia benchi jambo ambalo linamfanya kuhofia kuuwa
kiwango chake.
Amesema mpaka sasa hakuna timu ambayo imeonyesha nia ya kutaka kumsajili, lakini yeye ni mchezaji anayetegemea soka kuendesha maisha
yake hivyo kujua mapema kutamsaidia kuchagua sehemu sahihi ya kwenda au kujipanga kwa ajila ya msimu ujao.

Chapisha Maoni

 
Top