kuendelea wikiendi hii kwa michezo sita.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, Jumamosi Aprili
8, mwaka huu Mbeya City itashindana na Ndanda
ya Mtwara kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya
wakati Majimaji ya Songea itaialika African Lyon ya
Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Majimaji mjini
Songea mkoani Ruvuma.
Mechi nyingine kwa siku ya Jumamosi Aprili 8,
mwaka huu itakuwa ni kati ya Kagera Sugar na
JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani
Kagera wakati wakati siku ya Jumapili Aprili 09,
mwaka huu Stand United itakuwa mwenyeji wa
Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kambarage
mkoani Shinyanga.
Ligi inatarajiwa kuendelea Jumatatu Aprili 10,
mwaka huu kwa michezo miwili ambako Simba
itakuwa mgeni wa Mbao kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza ilihali Mtibwa Sugar itaialika
Azam FC kwenye Uwanja wa Manungu mkoani
Morogoro.
Jumamosi Aprili 8,2017
Mbeya City v Ndanda FC (Sokoine)
Majimaji FC v African Lyon (Majimaji)
Kagera Sugar v JKT Ruvu (Kaitaba)
Jumapili Aprili 09,2017
Stand United v Tanzania Prisons (Kambarage)
Jumatatu Aprili 10,2017
Mbao FC v Simba SC (Kirumba)
Mtibwa Sugar v Azam FC
Chapisha Maoni