0
KLABU ya Zamalek inayoshiriki ligi kuu ya nchini
Misri leo Ijumaa imemtangaza Mreno Augusto
Inacio kuwa kocha wake mkuu mpya.
Inacio mwenye umri wa miaka 67 ameingia
kandarasi ya mwaka mmoja na nusu ya
kuifundisha miamba hiyo ya jiji la Cairo akichukua
mikoba ya mzawa,Mohamed Helmy aliyetimuliwa
kibarua hicho hivi karibuni kutokana na
muendelezo wa matokeo mabovu.
Akifanya mahojiano mara baada ya kusaini
kandarasi hiyo,Inacio amesema atafanya kila
awezalo kuipa mafanikio makubwa klabu hiyo.
Kabla ya kutua Zamalek, Inacio aliwahi
kuvifundisha vilabu vya Rio Ave, Marítimo,Sporting
CP na Moreirense vya nyumbani kwao Ureno.Pia
aliwahi kuifundisha klabu vya Al Ahli SC ya nchini
Qatar.
Msimu uliopita ulikuwa ni wenye mafanikio zaidi
kwa Inacio kwani akiwa kocha msaidizi wa Porto
aliweza kutwaa ubingwa wa Taça da Liga (Kombe
la Ligi) baada ya kuifunga Braga kwenye mchezo
wa fainali.
Jumla Inacio ameshinda vikombe vitatu akiwa
kocha mkuu na vikombe vinane akiwa kocha
msaidizi.

Chapisha Maoni

 
Top