0
Liverpool wamethibitisha kuwa Fowadi wao Sadio
Mane hatocheza tena Msimu huu uliobaki baada
ya Jumamosi iliyopita kuumia Goti kwenye Mechi
waliyowachapa Everton 3-1.
Fowadi huyo kutoka Senegal mwenye Miaka 24 na
ambae ndie tegemeze kubwa la Liverpool na
ambae ndie aliewafungia Bao la Kwanza kwenye
Mechi hiyo na Everton aliumia baada kuvaana na
Leighton Baines wa Everton.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ana
hakika Mane anahitaji upasuaji na itakuwa ngumu
kwake kucheza tena Msimu huu unaokwisha
Mwezi ujao.
Mane, aliesainiwa kutoka Southampton kwa Dau
la Pauni Milioni 34, amecheza Mechi zote za
Liverpool Msimu huu kasoro 5 tu.
Kati ya Mechi hizo, 3 zilikuwa Sare na 2
wamefungwa na kuwaacha Liverpool wakiwa
Nafasi ya 3 kwenye EPL, Ligi Kuu England, wakiwa
na Pointi 60 kwa Mechi 31 wakiwa Pointi 12
nyuma ya Vinara Chelsea.
Fowadi huyo anaungana na Majeruhi wengine
Jordan Henderson na Adam Lallana ambao
wamepelekwa huko USA kwa matibabu zaidi.
Mchezaji mwingine alieumia kwenye Mechi hiyo
na Everton ni Kiungo Emre Can ambae
ameshindwa kufanya hata Mazoezi kutokana na
maumivu ya Goti.
Lakini habari njema kwa Liverpool ni kuanza tena
Mazoezi kwa Straika wao Daniel Sturridge ambae
kitambo yuko nje kwa maumivu na upo
uwezekano akawepo Benchi Jumatano wakiivaa
Bournemouth.

Chapisha Maoni

 
Top