0
Ni mechi ngumu kwa upande wa Wanajangwani
hasa kutokana na rekodi yao mbovu dhidi ya
timu kutoka upande wa kaskazini mwa Afrika
Yanga itashuka dimbani siku ya Jumamosi katika
uwanja wa taifa jijini Dar ea salaam kuwakabili
Mc Alger kutoka Algeria kwenye mchezo wa
awali wa kombe la shirikisho Afrika.
Yanga wanaitaji kushinda mchezo huo wa awali
kwa ajili ya kujitengenezea mazingira mazuri
kwenye mchezo wa marudiano utakao fanyakia
wiki moja badae nchini Algeria.
Ni mechi ngumu kwa upande wa Wanajangwani
hasa kutokana na rekodi yao mbovu dhidi ya
timu kutoka upande wa kaskazini mwa Afrika.
Maandalizi mazuri, utimamu wa mwili na kutumia
nafasi vizuri ndiyo silaha kwa Yanga kuibuka na
ushindi siku hiyo.
Goal inakuletea nyota wa Mc Alger ambao Yanga
wanatakiwa kuwa makini nao ili kufanikiwa
kuibuka na ushindi
ABDERAHMANE HACHOUD
Mlinzi wa kulia na ndiye nahodha wa kikosi cha
Mc Alger, anavalia jezi namba 27 mgongoni,
nyota huyo licha ya kucheza beki ila ndiye
mfungaji bora wa klabu kwenye Ligi Kuu nchini
mwao kwa mabao yake 4, ni mzuri kwenye
kupiga mipira iliyokufa, Yanga wanatakiwa kuwa
makini kucheza faulo za karibu ya goli lao la
sivyo mlinzi huyo anaweza kuwafunga kwa
mipira hiyo.
HICHEM NEKKACHE
Mshambuliaji wa kati mwenye jezi namba 9, ni
straika mjanja awapo eneo la timu pinzani, ni
mzuri kwenye mipira ya hewani na ile ya moja
kwa moja, mshambuliaji huyo hahitaji nafasi tatu
kufunga goli.
Safu ya ulinzi Yanga inaitaji kupunguza makosa
binafsi siku hiyo bila hivyo atawafunga.
HADJI BOUGUE'CHE
Ni mkongwe ndani ya kikosi akiwa na umri wa
miaka 33, hucheza nafasi tofauti-tofauti,
mshambuliaji wa kati au straika namba mbili,
licha ya umri mkubwa aliokuwa nyota huyo ni
mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi
hicho
BRAHIM BOUDEBOUDA
Mlinzi wa kushoto ndani ya Mc Alger mwenye
jezi namba 26, anaitaji kuwekewa mikakati mikali
pindi apandapo kusaidia mashambulizi, ni hatari
sana kwenye kupiga krosi pia ana uwezo
mkubwa wakufunga

Chapisha Maoni

 
Top