Mavugo amesema kipigo walichokipata kutoka
kwa Kagera Sugar hakitawakatisha tamaa bali
watazidi kujituma ili kufanikisha lengo lao la
ubingwa
Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo,
amesema kipigo walichokipata kutoka kwa
Kagera Sugar hakitawakatisha tamaa bali watazidi
kujituma ili kufanikisha lengo lao la ubingwa
msimu huu.
Mavugo ameiambia Goal, hali kama hiyo
hutokea kwa timu yoyote hivyo hawana haja ya
kukata tama kwasababu bado wanayo nafasi ya
kurekebisha makosa yao.
“Hatukucheza vizuri ndiyo maana hatukuweza
kupata matokeo lakini hivyo ni vitu vya kawaida
ambavyo hutokea kwenye soka, kitu cha msingi
tujipange ili tuweze kushinda mechi zinazokuja
mbele,” amesema Mavugo.
Mshambuliaji huyo rai wa Burundi pia amesema
kikwazo kikubwa kwenye mchezo huo ilikuwa ni
kipa Juma Kaseja ambaye aliweza kucheza vizuri
kwa kuokoa michomo yao mingi waliyopiga
kwenye lango la Kagera Sugar.
Amesema kama Kagera ingekuwa na kipa
mwenye kiwango cha kawaida basi wangeweza
kuibuka na idadi kubwa ya mabao lakini kila
walipojaribu walishindwa kufanya hivyo kutokana
na uhodari aliokuwa nao na kuwanyima ushindi.
Mavugo amewataka mashabiki wa timu hiyo
kutulia na kuendelea kuwasapoti ili waweze
kufanya vizuri kwenye mechi tano zilizosalia hasa
mbili watakazocheza Jijini Mwanza na timu za
Toto Africans na Mbao FC.
Chapisha Maoni