0
Lwandamina amesema amepanga kutumia
mfumo wa 4-3-3, kwa lengo la kujaza viungo
wengi huku akiwatumia Ngoma, Obrey Chirwa na
Haruna Niyonzima
Vinara wa Ligi Kuu, Yanga kesho watakuwa
nyumbani uwanja wa Taifa Dar es Salaam,
kuwakabili MC Alger ukiwa ni mchezo wa kwanza
wa katika hatua ya kuwania kufuzu hatua ya
makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho
Afrika CAF.
Hiyo ni nafasi muhimu kwa kocha George
Lwandamina, kuhakikisha anaipeleka timu hiyo
hatua ya makundi na hatimaye kucheza fainali ya
michuano hiyo kutokana na rekodi aliyokuwa
nayo msimu uliopita akiwa anaifundisha Zesco
United ya kwao Zambia.
Mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa mgumu kwa
pande zote hususani Yanga ambao watakuwa
wakicheza mbele ya mashabiki wao kitu ambacho
kitakuwa kinawaongezea presha ya kutaka
kushinda ingawa rekodi ya mabingwa hao
wanapocheza nyumbani kwenye michuano hiyo
huwa siyo mzuri.
Kocha Lwandamina ataingia kwenye mchezo huo
akijivunia kurejea kwa nyota wake waliokuwa
majeruhi akiwemo Donald Ngoma raia wa Zambia
pamoja na Amissi Tambwe ambao
wamekosekana kwa muda mrefu kwenye kikosi
chake.
Daktari wa Yanga Edward Bavo amemsibitishia
Lwandamina kuwa Ngoma yupo fiti kwa asilimia
100, kucheza kwenye mchezo huo ispokuwa
bado ana hofu na Tambwe ambaye licha ya
kuanza mazoezi lakini bado hajawa timamu
vyakutosha.
Kiungo Mzibabwe Thaban Kamusoko na Mzambia
Justine Zulu, wataendelea kukaa jukwaani
kuangalia mchezo huo kutokana na kuendelea
kuwa majeruhi lakini kurejea kwa Ngoma
kunaonekana kutuliza hofu ya mashabiki wa timu
hiyo kutokana na uhodari wa kupambana
aliokuwa nao nyota huyo.
Lwandamina amesema amepanga kutumia
mfumo wa 4-3-3, kwa lengo la kujaza viungo
wengi huku akiwatumia Ngoma, Obrey Chirwa na
Haruna Niyonzima kuweza kufunga na wakati huo
huo wawili kushuka chini kuja kusaidia ukabaji
pamoja na kuumiliki mpira kwa mua mrefu.
“Tumejiandaa vyakutosha na ninaimani kubwa na
wachezaji wangu, tunajua tunacheza na timu
kubwa na ngumu, lakini kwakua tupo nyumbani
tutapambana kuhakikisha tunashinda na kuwapa
furaha mashabiki wetu,’amesema Lwandamina.
MC Alger wameshawasili Tanzania usiku wa
kuamkia leo na leo jioni watafanya mazoezi
kwenye uwanja wa Taifa ambao ndiyo
utakaochezewa mechi hiyo muhimu kwa kila
upande.
Kocha wa MC Alger Kamel Mouassa, leo
amezungumza na waandishi wa habari na
amesema wamekuja Tanzania kushinda na hiyo
ni kutokana na kuwajua vizuri wapinzani wao
Yanga baada ya kuwafuatilia katika mechi zao za
hivi karibuni.
“Najua mchezo utakuwa mgumu lakini
tunattambua wapinzani wetu Yanga wana
matatizo na hawapo vizuri kutokana na matatizo
mbalimbali ikiwemo kiuchumi hivyo tutatumia
mapungfu hayo kuhakikisha tunawafunga na
kuwatoa,”amesema Mouassa.
Mshindi wa jumla kati ya timu hizo mbili atafuzu
moja kwa moja hatua ya makundi ya kombe la
Shirikisho Afrika na kuungana na timu nyingine
32 ambazo zitakuwa zimefuzu kwa hatua hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top